Suarez atoa zawadi ya krismasi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Luis Suarez

shambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez ametoa zawadi kwa watoto 500 na familia zao.

Zawadi hiyo ya Suarez kwa watoto hao walio hospitali pamoja na wazazi wao ni kwa ajili ya Krismasi.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool, amefikisha zawadi hiyo kwenye Hospitali ya Pereira Rossell mjini Montevideo, Uruguay.

Pamoja na kugawa zawadi hizo Suarez anayetambulika kwa utukutu, ameandika ujumbe mzuri wa kuwatakia sikukuu njema ya Krismasi, watoto hao pamoja na wazazi wao au wapendwa wao.