Chelsea kuchuana na West Ham

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chelsea

Harakati za Chelsea kuendelea kudhibiti uongozi katika ligi ya Uingereza utaendelea hii leo katika mechi za siku ya Boxing Dei zinazoshirikisha ligi za madaraja tofauti ya soka nchini Uingereza.

The Blues kama wanavyojulikana ambao wana alama tatu juu ya mabingwa wa ligi hiyo Manchester City watachuana na West Ham mwendo wa tisa na dakika 45 saa za afrika mashariki.

Ni mechi ya pili ya Chelsea katika mechi nne ndani ya siku 11.

''Haijalishi wewe ni muingereza ama si Muingereza pindi tu unapochezea kilabu yoyote nchini humo ,mimi nakuheshimu'', alisema Mourinho kocha wa Chelsea.

''Kwa sasa wachezaji wa Ujerumani wako katika fukwe za bahari,wale wenzao wa Uhispania wako katika visiwa vya Maldives wakiota jua na wengine pia wanafanya hivyo.Lakini nchini humu unacheza tarehe 22,unacheza siku ya Boxing dei,unacheza tarehe 28 na vilevile tarehe 31.Hakuna siku kuu ya krisimasi ni soka tu,na nadhani wachezaji wanahitaji kuheshimiwa'',

Baada ya mechi hiyo dhidi ya 'wananyundo' .Chelsea itatembelea Southampton tarehe 28 Disemba na Totenham tarehe 1 January Chelsea iliishinda Stoke 2-0 siku ya jumatatu ili kusalia na alama tatu juu ya Manchester City .