Van Gaal:Tunataka kushinda ligi

Haki miliki ya picha
Image caption Kocha wa Manchester Louis van Gaal

united Louis Van GaalManchester United bado ina matumaini ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu.

Kulingana na mkufunzi Louis Van Gaal lengo lao ni kushinda ligi hiyo msimu huu licha ya kuwa wako alama 10 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo sasa Chelsea.

Baada ya kuanza na matokeo mabaya, mashetani hao wekundu wameshinda mechi sita mfululizo kabla ya kutoka sare katika mechi ya saba.

''Lengo letu kuu ni kushinda ligi mwishoni mwa msimu huu'',alisema Van Gaal.