Crystal Palace yampiga kalamu kocha wake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Neil warnock aliyefutwa kazi na Crystal Palace kutokana na matokeo mabaya.

Neil Warnock amekuwa meneja wa kwanza wa ligi ya Uingereza kupigwa kalamu msimu huu baada ya kufutwa kazi na Crystal Palace.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 66 alijiunga na timu hiyo kwa mara ya pili mnamo mwezi Agosti mwaka 2014 kufuatia kuondoka kwa Tony Pulis.

Hatua hiyo inafutia kichapo cha mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Southampton siku ya boxing dei.

Palace kwa sasa iko katika eneo la kushushwa daraja ikiwa na alama moja juu ya Hull City ilioko katika nafasi ya 17.

Meneja msaidizi Keith Millen sasa atachukua fursa ya kuiongoza kilabu hiyo dhidi ya QPR siku ya jumapili.

Warnock alishinda michuano mitatu pekee kati ya mechi 16 alizosimamia.