Ushindani wazidi katika ligi ya EPL

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olivier Giroud alipewa kadi nyekundi katika ushindi wa arsenal dhidi ya QPR

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa Olivier Giroud alihitaji kupewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya QPR,lakini akathibitisha kuwa mshambuliaji huyo ameomba msamaha baada ya kisa hicho.

Giroud mwenye miaka 28 alionekana akimpiga kichwa Nedum Onuoha katika kipindi cha pili cha ushindi wa 2-1.

Wakati huohuo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa beki John Terry anacheza kama wakati alivyoiongoza the blues kushinda ligi ya Uingereza miaka kumi iliopita.

Ana motisha chungu nzima.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption John Terry alifunga bao la kwanza la Chelsea

''Sioni tofauti ya John wa miaka ya 2004,05,06 sioni tofauti yoyote'',alisema Mourinho.

Terry alifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham na kuifanya timu hiyo kusalia kileleni mwa ligi hiyo.

Kwengineko mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa ametosheka na uongozi unaotolewa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ambaye alicheza katika safu ya kati na kuisadia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rooney aliifungia Manchester United mabao mawili katika ushindi wa mabo 3-1 dhidi ya Newcastle

Rooney alifunga mabao mawili na kutoa usaidia wa bao la tatu kwa Robin Van Persie.

Nayo Manchester City ilifunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza dhidi ya West Bromwich licha ya barafu iliokuwa ikianguka katika uwanja huo na kusalia nyuma ya Chelsea kwa alama tatu.

Fernando aliifungia City bao la kwanza,baada ya Ben Foster kutoa kross nzuri kutoka kwa Jesus Navas.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Yaya Toure alicheka na wavu wa Westbromwich alipopiga mkwaju wa Penalti

Yaya Toure alifunga bao la pili kupitia mkwaju wa Penalty kabla ya David Silva kufunga bao la tatu.

West Bromwich walifunga bao la kufutia machozi wakati wa kipindi cha pili.

Hivi ndivyo ilivyokuwa:

Chelsea 2 - 0 West Ham

Burnley 0 - 1 Liverpool

Crystal Palace 1 - 3 Southampton

Everton 0 - 1 Stoke

Leicester 1 - 2 Tottenham

Man Utd 3 - 1 Newcastle

Sunderland 1 - 3 Hull

Swansea 1 - 0 Aston Villa

West Brom 1 - 3 Man City

Arsenal 2-1 QPR