Chelsea na Man U wapata kibarua kigumu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambuliaji wa Manchester United Robie Van Persie akifunga bao

Mlinda lango wa Totenham Hugo Lioris yuko tayari kuchukua mahala pake Dhidi ya Manchester United licha ya kuuguza jeraha katika mdomo wake wakati wa ushindi dhidi ya Leicester.

Ryan Mason pia anatarajiwa kurudi katika kikosi cha kwanza baada ya kucheza dakika 45 kama mchezaji wa ziada siku ya boxing dei.

Kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria hajulikani iwapo atashiriki mechi hiyo kufuatia jereha alilopata siku moja tu kabla ya krisimasi.

Image caption Mchezaji wa Southampton wanyama

Kwengineko, beki wa Manchester City Vincent Kompany huenda akarejea katika kikosi dhidi ya Burnley baada ya kukosa mechi mbili kutokana na jeraha la paja.

City pia itamchunguza mshambuliaji Stevan Jovetic aliye na jeraha la mguu baada ya kutotumiwa siku ya boxing dei.

Kwa upande wake Burnley itamkosa beki Michael Duff na Stephen ward.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Beki wa Mancity Vincet Kompany

Wakati huohuo kocha wa Chelsea Jose Mourinho hana wasiwasi wa majeraha mapya.

Didier Drogba,Fillipe Luis,Andre Schurrle na John Obi Mikel huenda wakashiriki iwapo the blues inataka kubadilisha kikosi chake dhidi ya Southampton.

Wachezaji wawili wa West Ham Alex Song na Diafra Sakho waligeuzwa katika kikosi cha kwanza dhidi ya Chelsea lakini sasa wanatarajiwa kurudi dhidi ya Arsenal.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa Chelsea Didier Drogba

Upande wa Arsenal mshambuliaji Olivier Giroud anaanza kuhudumia marufuku yake ya mechi tatu hatua ambayo itamfanya Danny Welbeck kuanza kama mshambuliaji wa katikati.

Gunners pia itamchunguza beki wa kati Laurent Koscielny ambaye anakaribia kurudi kikosini kutokana na jeraha la mguu.