Keith Millen meneja wa Crystal Palace?

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kocha wa Muda wa Crystal Palace Keith Millen

Kocha wa muda wa timu Crystal Palace Keith Millen yuko tayari kuchukua jukumu la kuifundisha timu hiyo kama kocha wa kudumu.

Millen anakaimu nafasi ya umeneja kwa muda baada ya kocha mkuu Neil Warnock kutimuliwa ,amekua na uzoefu wa kukiongoza kikosi hicho baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza ni pale Tony Pulis alipoikacha timu hiyo mwanzoni mwa msimu.

"Niko tayari kuwa kocha wa kudumu wachezaji wananiheshimu kwa ufahamu wangu, na kufanya kazi kwa bidii nimefanya hivi mara kadhaa pamoja nao".

Pia kumekua na tetesi kocha Alan Pardew anaweza pewa nafasi ya kuwa kocha mpya katika klabu hiyo ya kusini mwa londoni.