Vigogo wa Ligi England waambulia sare

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Manchester United dhidi ya Tottenham

Vigogo Manchester City,Chelsea na Man United wamejikuta wakiambaulia sare katika michezo yao ya ligi ya England.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Manchester City waliambulia sare baada ya kuruhusu timu ya Burnley kurudisha mabao mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.

Huku vinara wa ligi hiyo Chelsea wakipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton. Sadio Mane aliipa Southampton Bao la kuongoza kabla ya Eden Hazard kuisawazisha timu yake Sekunde chache kabla ya mapumziko.

Manchester United wakiwa ugenini kwenye uwanja wa White Hart Lane walishindwa kutamba mbele ya Tottenham kwa kukubali kutoka sare ya 0-0.

Matokeao ya michezo mingine

Aston Villa 0 - 0 Sunderland

Hull City 0 - 1 Leicester City

Queens Park Rangers 0 - 0 Crystal Palace

Stoke City 2 - 0 West Bromwich Albion

West Ham United 1 - 2 Arsenal

Newcastle United 3 - 2 Everton

Matokeo haya bado yanawabakisha Chelsea kileleni mwa Ligi mbele ya Timu ya Pili Mabingwa Watetezi Man City wakifuatiwa na Man United waliuoko nafasi ya tatu.