Azam ,Yanga na Mtibwa wakubali sare

Image caption watani wa jadi wakiumana

Ligi kuu ya Tanzania iliyoingia kwenye mzunguko wa pili ilianza kwa kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali mwishoni mwa juma.

Simba Sc walianza mzunguko wa pili vibaya baada ya kukubali kichapo cha bao1-0 dhidi timu ya Kagera Sugar toka mkoani kagera.

Mabigwa watetezi Azam Fc waliokua wageni wa Yanga walifanikiwa kusawazisha bao na mchezo kumalizika kwa sululu ya mabao 2-2 mchezo ulichezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

katika uwanja wa SokoineMbeya , ilipata ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara, Polisi Moro waliibuka kidedea kwa kuichapa Mgambo Jkt 2-0.

Vinara Mtibwa walishindwa kutamba mbele ya Stand United kwa kukubalim sare ya 1-1, Ruvu Shooting walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao JKT Ruvu.

Ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano kuchezwa.

Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini.

Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.