Clarke alikua na kesi kabla ya ajali

Image caption Clarke Carlisle

Mcheza mpira wa zamani Clarke Carlisle alishitakiwa kwa kosa la la kuendesha gari akiwa amelewa siku chache kabla ya kupata ajali mbaya ya kugongana roli.

Carlisle mwenye umri wa miaka 35 alipata ajali tarehe 22 na bado yuko Hospital mjini Leeds.

Polisi wa Metropolitan wamethibitisha alikua na shitaka la kuendesha akiwa kalewa mnano tarehe 20 Desemba. Na alitakiwa kufika mahakama ya Highbury Corner tarehe 20 januari .

Clarke Carlisle alivichezea vilabu vya Burnley, Queens Park Rangers, Leeds United na Northampton Town, na pia alikua mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa kulipwa.

Mke wake Gemma aliandika kwenye mtandao wa twita siku ya jumatatu"Hali yake bado ni mbaya ila tunaimani atapona tunashukuru kwa msaada wenu.