Kombe la Mapinduzi kuanza Januari Mosi

Image caption Timu ya Kmkm ya Zanzibar moja kati ya washiriki

Michuano ya kombe la mapinduzi kuanza kutimua vumbi Zanzibari kuanzia januari mosi mpaka Januari 13 mwakani.

Hii itakua ni mara ya tisa kufanyika tangu ianzishwe kuenzi Mapindunzi ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964.

Timu zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Yanga Sc, Azam Fc,Simba Sc na Mtibwa Sugar.

Wenyeji watawakilishwa na mabingwa wa Zanzibar KMKM, Police FC, JKU, Mtende Rangers na Shaba FC.

KCC FC ya Uganda watashiriki pia michuano hiyo wakiwa ni mabigwa watetezi wa kombe hilo.

Timu waalikwa toka nchini kenya zilizoalikwa kushiriki michuano hii zimejitoa.