Michael van Gerwen atinga nane bora

Image caption Michael Van Gerwen

Mchezaji wa mchezo wa Vishale Michael van Gerwen,amefanikiwa kuingia hatua ya nane bora katika michezo ya dunia kwa kumfunga Terry Jenkins kwa mabao 4-1

Katika michezo mingine Robert Thornton pia aliibuka kidedea kwa kumchapa Benito van de Pas kwa mabao 4-0 na atachuana na Van Gerwen katika hatua ya robo fainali.

Raymond van Barneveld alifanikiwa kuingia robo kwa kupata ushindi wa 4-3 dhidi ya mpinzani wake Jamie Caven.

Huku Stephen Bunting akishinda kwa ushindi wa 4-1 mbele ya James Wade, Mwingereza Smith alipata ushindi licha ya kutanguliwa kwa 2-0 kwenye awamu ya kwanza na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Brendan Dolan.

Mchezaji wa Uholanzi Vincent van der Voort alimaliza kwa kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 kwa kumtwanga Max Hopp toka Ujerumani.