Kobe Bryant aanza vibaya NBA

Image caption Kobe Brayant

Mchezaji nguli wa mchezo wa kikapu Nchini Marekani Kobe Bryant amerejea vibaya katika kikosi chake cha LA Lakers kwa kukubali kichapo cha vikapu 116 -107 – toka kwa Phoenix Suns.

Kobe alikua anareje uwanja ni baada kukosa michezo mitatu iliyopita, alifunga pointi 10 ribaundi 8 na akisaidia kutoa pasi 7 za mwisho za vikapu.

Goran Dragic aliifungia Phoenix Suns pointi 24 na Eric Bledsoe akiongeza pointi 22

Matokeo mengine ya NBA yalikua Cleveland Cavaliers 80 - 103 Detroit Pistons ,San Antonio Spurs 110 - 106 Houston Rockets ,Dallas Mavericks 112 - 107 Oklahoma City Thunder, Denver Nuggets 102 - 116 Toronto Raptors ,Portland Trail Blazers 101 - 79 New York Knicks.