Alan Ivrine afukuzwa kazi West Brom

Image caption Alan Ivrine

Timu ya West Brom imemfuta kazi kocha wake Alan Ivrine ambaye amekuwa na klabu hiyo kwa miezi saba tangu apate kibarua hicho.

Kocha huyo mwenye miaka 56 raia wa Scotland alikuwa na mkataba wa miezi 12 ambaa upo katika mfumo wa uendelevu.

Ivrine alichukua nafasi ya Pepe Mel ambaye alikuwa akikinoa kikosi hicho ambapo kwa sasa mfululizo vipigo na hiki cha Jumapili cha 2-0 toka kwa Stoke City kimeuchefua timu hiyo na kuona iko haja kocha huyo kuachia ngazi.