Wanariadha wanaotumia dawa mashakani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanariadha wa kenya

Wanariadha watakaopatikana wametumia dawa za kusisimua misuli watapigwa marufuku ya miaka minne kulingana na sheria mpya ya kukabiliana na tatizo hilo inayoanza kufanya kazi hii leo.

Lakini sheria hiyo ya kimataifa ambayo inashirikisha sheria zote za michezo duniani inasema kuwa marufuku hiyo inaweza kupunguzwa kwa wanariadha ambao wataonyesha kwamba hawakuwa na lengo la kufanya udanganyifu ama ambao wako tayari kuwasaidia wachunguzi kuwagundua wanariadha wengine wanaotumia dawa za kusisimua misuli.

Sheria hiyo pia inatoa adhabu kali kwa wale wanaokwepa uchunguzi wa dawa hizo huku wanariadha wanaofanya hivyo wakipewa marufuku ya miaka miwili kwa wachezaji wanaokosa kuchunguzwa mara tatu katika kipindi cha miezi 12.