Mancity yafika kileleni mwa ligi ya EPL

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Manchester City yafika katika kilele cha uongozi wa ligi ya EPL baada ya kuishinda Sunderland 3-2

Mchezaji Frank Lampard alifunga bao la ushindi kupitia kichwa chake dhidi ya Sunderland na kuiweka Manchester City sawa na Chelsea katika kilele cha ligi ya Uingereza.

Mabao ya Yaya Toure na Steven Jovetic yaliifanya Manchester City kudhibiti mechi hiyo.

Lakini timu hiyo ya nyumbani ilipoteza uongozi huo wa mabao mawili kwa mechi ya pili mfulululizo kupitia mabao ya Jack Rodwell na penalti ya Adam Johnson iliosawazisha.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mchezaji Frank Lampard aliyeifungia Manchester City bao la ushindi.

Lampard alifunga bao la ushindi kupitia kichwa kizuri baada ya kupata krosi kutoka kwa Gael Clichy.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea ambaye atasalia katika timu hiyo baada ya Mancity kumuongezea mkataba hadi mwisho wa msimu kutoka New York City nusra afunge mabao matatu katika dakika 20 alizokuwa uwanjani ambapo City ilimaliza mechi hiyo kwa kishindo.