Alan Pardew ajiunga na Crystal Palace

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyekuwa kocha wa Newcastle Alan Pardew amejiunga na Crystal Palace kama mkufunzi wake mpya

Kilabu ya Crystal Palace imemsajili kocha wa Newcastle Alan Pardew kama meneja wao.

Pardew alipewa rukhsa na Newcastle kuzungumza na kilabu hiyo ya London baada ya klabu hizo mbili kukubaliana kuhusu fidia siku ya jumatatu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 anachukua mahala pake Neil Warnock ambaye alifutwa kazi jumamosi iliopita ikiwa ni miezi minne tu tangu aajiriwe na kilabu hiyo.

Kilabu ya Palace bado haijathibitisha mktaba huo lakini BBC inaelewa kwamba Pardew aliweka kandarasi na kilabu hiyo mpya siku ya ijumaa jioni.

Pardew alikuwa akishuhudia mechi ambapo Palace ilipata sare ya 0-0 katika uwanja wa Villa Park siku ya mwaka mpya ,matokeo yalioiweka katika eneo la kushushwa ngazi .