Kocha: Ronaldo atarudi Old Trafford.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Christiano Ronaldo akisherehekea bao lake dhidi ya Barcelona

Aliyekuwa msaidizi wa kocha wa Manchester united Mike Phelan anaamini kuwa Cristiano Ronaldo huenda akaandikisha mkataba wa kurudi katika kilabu ya Old Trafford katika siku sijazo.

Ronaldo amehusishwa na mpango wa kurudi Manchester United katika muda wake katika kilabu ya Real Madrid ,lakini mpango kama huo haujazaa matunda kufikia sasa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye alichezea Man U anafurahia maisha yake katika kilabu ya Real Madrid lakini Phelan anaamini huenda akashawishika kurudi katika ligi ya Uingereza.