Arsenal,Mancity na Man U kuwania FA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Theo walcot

Mshambuliaji wa Uingereza Theo Walcot anatarajiwa kuanza katika mechi ya leo ya raundi ya tatu ya kombe la FA dhidi ya Hull City.

Mlinda lango David Ospina anatarajiwa kuchukua mahala pake Wojcieh Sczesny katika mechi ya jumapili katika uwanja wa Emirates,huku Mesut Ozil akitarajiwa kuanza mazoezi baada ya kupata jeraha.

Na huku hayo yakijiri wachezaji kadhaa wa Chelsea huenda wakapumzishwa katika mechi dhidi ya Watford.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kipa wa Chelsea Petr Cech

Kipa Thibaut Courtois ana jeraha la kidole,hivyobasi huenda kipa mwenye uzoefu mwingi Petr Cech akachukua mahala pake.

Mshambuliaji Diego Costa na kiungo wa kati Eden Hazard huenda wakawachwa nje baada ya kushiriki katika mechi nyingi za ligi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiungo wa kati wa Mancity Yaya Toure

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure huenda akashiriki mechi yake ya mwisho kabla ya kujiunga na kikosi cha Ivory Coast kwa kombe la Afrika.

Beki Vincent Kompany , Edin Dzekona Sergio Aguero wana majeraha ya mguu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa Manchester United

Timu ya daraja la kwanza Yeovil inataraji kwamba mshambuliaji wake Kieffer Moore atakuwa tayari kucheza katika mechi dhidi ya Manchester United.

Moore alifunga bao la pili dhidi ya Accrington katika mechi ya raundi ya pili iliochezwa disemba 16 lakini hajacheza hadi sasa.