Song astaafu soka ya kimataifa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchezaji wa West Ham Alex Song amestaafu katika soka ya kimtaiafa baada ya kukosa kujumuishwa katika kikosi kitakachoiwakilisha nchini hiyo huko Equitorial Guinea

Mchezaji wa Cameroon West Ham Alex Song amestaafu kucheza soka ya kimataifa baada ya kutopata mwaliko wa kikosi cha timu ya taifa kitakacholiwakilisha taifa hilo katika kombe la nchi za Afrika.

Song mwenye umri wa 27, ambaye kwa sasa anachezea timu ya ligi kuu ya Uingereza West Ham kupitia mkopo wa Barcelona sasa ataweza kuendelea kuichezea West Ham baada ya mazungumzo ya dakika za mwisho na Cameroon kuvunjika.

Song hajaichezea timu yake ya taifa tangu alipopewa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Croatia katika ngazi ya makundi katika Kombe la Dunia 2014.