Jose Mourinho matatani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jose Mourinho

Bosi wa timu ya Chelsea Jose Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la kimataifa la soka FA kwa madai yake kwamba kuna kampeni ya chinichini inayofanywa na marefa dhidi ya timu yake

Kauli hiyo ya Mourinho aliitoa baada ya kutoridhishwa na penati ilisababisha timu yake itoke sare ya moja moja na Southampton ,mwezi uliopita mnamo tarehe 28.

Mourinho ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu na amepewa muda mpaka tarehe 13 ya mwezi huu kujibu tuhuma zinazomkabili.