Bony kuhamia Mancity kwa £30m

Haki miliki ya picha gett
Image caption Wlfried Bony

Kilabu ya Uingereza Swansea City imekubali ada ya uhamisho ya takriban pauni milioni 30 kutoka kwa Manchester City ya kumnunua Wilfried Bony, 26.

Meneja wa Swansea, Gary Monk amesema kuwa itahitaji "kitita cha ajabu" kumhamisha Bony kutoka Swansea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wilfried bony na Kocha wa Swansea

Alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika mabao 20.

Bony alijiunga na Swansea mwaka 2013 kutoka Vitese Arnhem kwa pauni milioni 12.

Mchezaji huyo kwa sasa yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.