Ronaldo atwaa tuzo ya FIFA Duniani 2015

Haki miliki ya picha AP
Image caption Cristiano Ronaldo mara baada ya kupatiwa tuzo yake

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameibuka mshindi katika tuzo ya FIFA kama mwanasoka bora duniani mwaka huu Ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.

Tuzo hii iliwajumuisha wachezaji wa soka watatu ambao Lionel Messi, Manuel Neuer na Ronaldo ambaye ameibuka mshindi.

Na mfungaji goli zuri la mwaka tuzo hiyo imechukuliwa na mwanasoka kutoka nchini Colombia James Rodriguez ambapo goli hilo lililovunja rekodi ni lile alilofunga Colombia dhidi ya Uruguay mwaka 2014 katika kombe la dunia.