Van Gaal ajitetea kuhusu Falcao

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal

Kocha wa Man United Louis Van Gaal amesema uamuzi wa kumuondoa mshambuliaji Radamel Falcao kutoka kwenye kikosi chake ulikuwa wa kiufundi.

Falcao ambaye alicheza mechi tano za awali, alishuhudia timu yake ikipoteza mchezo kwa bao 1-0 walipokutana na Southampton hapo jana wakiwa Old Trafford.

Falcao anaichezea manchester kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu akitokea Monaco lakini amefunga magoli matatu pekee tangu alipojiunga na Manchester mwezi Septemba mwaka jana