Sijui nitacheza wapi msimu ujao:Messi

Image caption Nahodha wa Argentina Lionel Messi

Hatima ya Nahodha wa Agentina Lionel Messi kusalia katika klabu yake ya barcelona bado iko mashakani.

Mashaka ya Messi kuendelea kuitumikia timu yake imekuja baada ya kauli yake aliyoitoa wakati wa utoaji wa tuzo za mchezaji bora wa dunia.

“Sijui nitacheza wapi msimu ujao, japo kuwa nimekua nikisema nataka kumaliza soka langu hapa Barcelona”.

Kauli hii imekuja siku chache baada ya kusema hana mpango wa kujiunga na timu yoyote kati ya Chelsea na Manchester City zinazomuwania.

Taarifa za kutokuelewana na kocha wake Luis Enrique ndio inaonekana chanzo cha Messi kutaka kuondoka katika klabu hiyo iliyomkuza.

Mkataba wa sasa wa Messi unatarajia kufika kikomo mwaka 2019, Timu za Manchester United na Real Madrid ndio pekee wanaoweza kumsajili messi kwa sababu za kifedha za kutumia kadri upatavyo.