Yaya Sanogo atua Crystal Palace

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Yaya Sanogo ametokea Arsenal kuelekea Crystal Palace

Timu ya Crystal Palace imemsajili kwa mkopo mshambuliaji Yaya Sanogo toka Arsenal mpaka mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa timu hiyo Alan Pardew toka atoke Newcastle.

Kulikua na tetesi angejiunga na klabu ya Bordeaux ya Ufaransa ambapo kocha wake Arsene Wenger alitaka kumtoa kwa timu za nje ya ligi ya Uingereza.

Sanogo mwenye Miaka 21 ameichezea Arsenal michezo mitano msimu huu na kufuga goli katika mchezo wa klabu bigwa dhidi ya Borussia Dortmund.

"Tunatampa nafasi , anahitaji kucheza michezo mingi Zaidi nafikiri yuko tayari na alithibitisha hilo akiwa na timu yake," Aliezea kocha Alan Pardew.