Kipande cha Jules Rimet chapatikana

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kombe la dunia la mwaka 1930 likijulikana kama Jules Rimet

Kipande kombe halisi la dunia la kwanza kimepatikana katika chumba cha kuhifadhia vifaa vya michezo cha Fifa makao makuu ya ofisi hiyo zilizoko Zurich, Uswiss.

Kombe hilo Jules Rimet kwa juu linabeba majina ya washindi wanne wa kwanza wa kombe la dunia kati ya mwaka 1930 na 1950.Ikumbukwe kwamba Uruguay na Italia ndio washindi pekee wa kwanza wa kombe la dunia kati ya 1930 na mwaka 1950.

David Ausseil, ni mbunifu wa makumbusho ya Shirikisho la soka duniani anaeleza kuwa kombe hilo la dunia lilipewa sura mpya ,na ana uhakika kwamba hakuna raisi yeyote wa Fifa aliyewahi kuliona kombe Jules Rimet .

Kombe hilo ambalo liliundwa kwa dhahabu tupu lilikabidhiwa kwa timu ya Brazil baada ya kufanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika kombe la dunia mwaka 1970 lakini liliibwa mnamo mwaka 1983 na halikuonekana tena na inadhaniwa kuwa sehemu ya juu ya kombe hilo la awali la dunia ilipotelea Brazil. .

Kulisaka kombe hilo ni sawa na kumtafuta mwanamke wa Misri,na huwezi kulipiga bei kwakuwa ni dhahabu ya familia.Kombe Jules Rimet lina urefu wa mita kumi na kombe hilo la zamani litawekwa kwenye maonesho katika makumbusho ya shirikisho hilo huko Zurich,maonesho yalopangwa kufanyika mwezi March mwaka 2016.

Uruguay ilishinda kwa mara ya kwanza kombe la dunia mwaka 1930 na kupokonywa ubingwa huo na Italia mwaka 1934 na 1938 ,kombe hilo halikushindaniwa tena mpaka baada ya vita vikuu vya pili vya dunia mwaka 1950,ambapo Uruguay ililitwaa tena kombe hilo.Jules Rimet ndiye raisi wa kwanza wa Shirikisho la soka duniani aliyekuwa madarakani mwaka 1921 hadi 1954.

Historia ya Kombe hilo iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1928, wakati Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wakati huo, Jules Rimet, alipoamua kuandaa michuano mikubwa zaidi duniani inayohusisha mataifa mbalimbali. Ufunguzi wa mashindano hayo ulifanyika miaka miwili baadaye (mwaka 1930) nchini Uruguay, wakati timu 13 zilipoalikwa kushiriki.

Kabla ya michuano ya Kombe la Dunia, mechi ya kwanza ya kimataifa ya soka duniani ilichezwa mwaka 1872 ikizihusisha England na Scotland. Kipindi hicho ilikuwa ni mara chache kwa mchezo wa soka kuchezwa nje ya Uingereza.

Hata hivyo, kuanzia mwaka 1900 mchezo wa soka ulipata umaarufu duniani kote na vyama vingi vya soka vikaanzishwa. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa kuchezwa nje ya Uingereza ilikuwa kati ya Ufaransa na Ubelgiji iliyochezwa Paris, Mei 1904.

Mchezo huo ulileta msukumo wa kuanzishwa kwa FIFA Mei 22, 1904. Shirikisho hilo lilianzishwa na vyama vya soka vya Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, Uholanzi, Hispania, Sweden na Uswisi huku Ujerumani ikiomba kujiunga.

Mwaka 1928, FIFA ilichukua uamuzi wa kuandaa michuano yao. Huku Uruguay ikiwa imeshinda mara mbili michuano ya Olimpiki na ikijiandaa kusherehekea mwaka mmoja baada ya kupata uhuru, FIFA iliamua kuipa Uruguay uenyeji wa michuano hiyo ya kwanza ya Kombe la Dunia mwaka 1930.