Paula Radcliffe,kubwaga manyanga riadha

Image caption Paul Radcliffe kubwaga manyanga riadha

Mwanariadha nguli wa Uingereza Paula Radcliffe anatarajiwa kustaafu mchezo wa kufukuza upepo rasmi mwezi April mwaka huu.

Radcliffe mwenye umri wa miaka 41ni mshindi wa mara tatu wa riadha London ambapo mara ya mwisho alishinda kwa baada ya kukimbia maili 26 huko Berlin Septemba 2011

Hata hivyo Radcliffe alivunja rekodi ya Dunia baada ya kukimbia kwa saa mbili na dakika 15 na sekunde 25 katika michuano ya mjini London ya kufukuza upepo mwaka 2005

"tunafarijika sana kuwa Paula amechagua London kwaajili yam bio zake za mwisho za kustaafu” amesema mwandaaji wa mashindano hayo.