Fainali za tenesi zapigwa Tanzania

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mchezo kazini

Michuano ya kimataifa ya tenesi kwa kanda ya Afrika kwa vijana chini inayofanyika Jijini Dar es salaam Tanzania yamefikia hatua ya fainali ya kwanza.

Katika fainali ya mchezaji mmoja mmoja Sada Nahiman wa Burundi alimfunga Mandi Juma Furaji wa Tanzania kwa seti 6-4 7-5.

Huku Abdoulshakur Kabura wa burundi akipata ushindi kwa seti 4-6 6-4 6-4 dhidi ya Damien Laporte wa Seychelles.

Katika michezo mingine Ernest Habiyambere wa Rwanda amemchapa Emanueli Malya wa Tanzania kwa jumla ya seti 4-6 7-6 na 6-4.

Yabsira Kadebe wa Ethiopia ameibuka kidedea kwa kumchapa Radjabu Ntambi wa Burundi kwa 6-2 6-2.

Kwa upande wa fainali ya wawili wawili Abdoulshakur Kabura na Jonathan Mugisha wa burundi wamewachapa Ryan Randiek na Keen Shan wa Kenya kwa seti 6-1 6-2.

Abraham Adelin na Georgina Kemmy wa Tanzania wamepata ushindi wa seti 6-1 6-1 dhidi ya Mwamini Bitungwa na Mariam Mujawiana wa Burundi

Michuano hii inayojumuisha wavulana na wasichana imegawanyika katika makundi matatu kutokana na umri Miaka kumi na sita , kumi na nne, na kumi na mbili.

Washindi watano wa jumla toka katika kila kundi wataenda kushiriki michuano ya tenesi ya Afrika kwa vijana itayofanyika Nchini Tunisia mwezi Machi.