Chelsea yaipa kichapo Swansea

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Diego Costa

Chelsea imeimarisha uongozi wake katika ligi ya Uingereza baada ya kuicharaza kilabu ya Swansea mabao 5 bila jibu katika mechi iliodhibitiwa na chelsea kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar ndiye aliyefungua mtiririko huo wa mabao alipofunga sekunde chache tu baada ya mechi kuanza.

Mshambuliaji hatari wa Chelsea Diego Costa alifanya mambo kuwa magumu kwa Swansea baada ya kupachika bao la pili katika dakika ya 20 kabla ya kuongeza bao jengine katika dakika ya 34.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Fellaini

Oscar alifunga bao lake la pili na kuiweka Chelsea mbele na mabao 4-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili Swansea ilijitahidi na kiweza kukosa mabao ya wazi lakini ilipofikia dakika ya 79 Schurlle alipafunga bao la tano.

Katika mechi nyengine Manchester United imeibuka mshindi kufuatia msururu wa matokeo mabaya baada ya kuichapa QPR mabao 2-0.

Marouane Fellaini na James Wilson walifunga mabao hayo yaliokuja katika kipindi cha pili katika uwanja wa Loftus Road.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption liverpool

Nayo Liverpool iliendelea kumpa presha kocha wa Aston Villa Paul Lambert baada ya kuishinda Aston Villa na hivyobasi kupata ushindi wa tatu mfululizo.

Borini alifunga bao la kwanza katika dakika ya 24 kabla ya lambert kumaliza kazi katika dakika ya 79.

Haya ndio matokeo ya mechi za jumamosi

Aston Villa 0 - 2 Liverpool

Burnley 2 - 3 Crystal Palace

Leicester 0 - 1 Stoke

QPR 0 - 2 Man Utd

Swansea 0 - 5 Chelsea

Tottenham 2 - 1 Sunderland