Ghana vs Senegal:Gyan na Sakho kutocheza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Asamoah Gyan

Huku Ghana na Senegal zikichuana katika mechi ya leo kundi la C,Wachezaji wawili muhimu katikja mechi hiyo huenda wasicheze kiputo hicho kinachongojewa kwa hamu na gamu

Nahodha wa timu ya Ghana Asamoah Gyan anaugua maradhi yanayosemekana kuwa ni malaria huku Mshambuliaji wa Senegal Diafra Sakho akidaiwa kuugua maumivu ya mgongo.Vilevile Timu hiyo ya Senegal huenda ikamkosa mchezaji Sadio Mane wa kilabu ya Southampton ambaye anauguza jereha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Diafra Sakho akiifungia kilabu yake ya West Ham

Shirikisho la soka la Ghana limetoa maelezo kuwa Gyan alikuwa amepumzishwa hospitali katika mji wa Mongomo tangu Jumamosi jioni na kuruhusiwa Jumapili asubuhi ,na inaelezwa kuwa maradhi hayo yametibiwa katika hatua za awali na mchezaji huyo anaendelea vyema.

Kukosekana kwa Gyan katika kikosi cha taifa lake, kunaweza kuwa mtihani kwa kocha wake mpya wa Ghana Avram Grant aliyewahi kuwa boss wa Chelsea ambaye lengo lake ni kuona Black Stars inapata ushindi dhidi ya Senegal.

Lakini walau analo chaguo, anaweza kumwita mchezaji wa timu ya Marseille ,mchezaji wa mbele Andre Ayew na pia mchezaji wa timua ya Everton Christian Atsu ama hata Mubarak Wakaso wa timu ya Celtic.