Arsenal yawashangaza mabingwa wa EPL

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Santi Carzola

Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.

Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.

Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mancity

Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.

Matokeo hayo yameiwacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.

City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo mwezi Septemba.