Algeria vs Afrika kusini:Ukweli wa mambo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kombe la mataifa ya Afrika

Afrika kusini haijafungwa na Algeria katika michuano miwili kati ya timu hizo baada ya kuishinda Algeria 2-1 mwaka 1996 na baadaye kupata sare ya 1-1 mwaka 2000.

Hatahivyo Bafana Bafana imeshinda mechi moja kati ya mechi 12 katika mashindano haya ,ijapokuwa haijashindwa katika mechi tano kufikia sasa tangu ianzishe kampeni zake za kufuzu kwa dimba la mataifa ya Afrika mwaka uliopita.

Nayo timu ya Algeria kwa jina maarufu 'The desert warriors imepata sare moja na kupoteza mechi 4 kati ya tano katika mashindano ya mataifa ya Afrika tangu ushindi wao maarufu wa mabao 3-2 dhidi ya Ivory Coast mwaka 2010.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mechi ya kombe la mataifa ya Afrika

Algeria imeshinda kufunga katika mechi hizo nne kati ya tano na hivyobasi kuwa na idadi ya mabao mawili kwa jumla.

Katika mechi 3 zilizochezwa kati ya mataifa haya mawili ,algeria haijawahi kushinda mechi hata moja.

Je, unatabiri nini katika mechi ya leo? kwa maoni yako basi Ingia katika mtandao wetu wa facebook katika bbcswahili.