Messi ang'ara dhidi ya Deportivo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Messi akifunga mojawapo ya mabao yake matatu dhidi ya Deportivo la Coruna

Mshambuliaji Lionel Messi wa Barcelona aliifungia timu yake mabao matatu dhidi ya Deportivo La Coruna ugenini na kuibuka na ushindi wa 4-0.

Baada ya ushindi huo Barca wamewasogelea vinara wa ligi Real Madrid wakiwa nyuma kwa pointi moja ingawa wamecheza mechi moja zaidi.

Messi sasa amewahi kufunga mabao matatu kwa mpigo mara 30 katika mechi zote alizocheza na 22 katika ligi ya Uhispania na hivyobasi kuzifikia rekodi zilizowekwa na wachezaji wakongwe akiwemo Alfredo Di Stefano na Telmo Zarra.

Cristiano Ronaldo ambaye anaonekana kama mpinzani wa Messi katika uchezaji soka duniani anaongoza kwa kupiga kwa kufunga mabao matatu kwa mpigo mara 23.

Awali Real Madrid iliichapa Getafe 3-0 huku mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo akifunga mabao 2.Mabingwa watetezi Atletico Madrid waliichapa Granada 2-0.