Senegal yaibwaga Ghana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Senegal yaichapa Ghana

Mshambuliaji wa Senegal Moussa Sow alifunga bao la mda wa lala salama na kuisaidia Senegal kupata ushindi dhidi ya Black stars ya Ghana.

Mchezaji huyo aliyeingia dakika za mwisho za mechi hiyo alifunga bao lake kunako dakika ya 90 na kuipatia timu yake alama zote tatu.

Mchezaji wa Ghana Andrew Ayew alifunga mkwaju wa Penalti baada ya kiungo wa kati wa Everton Christian Atsu kuangushwa katika eneo la hatari.

Lakini Senegal ilijitahidi na kupiga chuma cha goli la Ghana kupitia mchezaji Kara Mbodj,kabla ya mshambuliaji wa Stoke Mame Biram Diouf kufunga bao la kusawazisha huku Mousa Sow akifunga bao la Ushindi.