Kikosi cha Guinea kumkosa nahodha wake

Haki miliki ya picha BEHROUZ MEHRIAFP
Image caption kikosi cha Guinea

Timu ya taifa ya Guinea itamkosa nahodha wake Kamil Zayatte, ambaye ana matatizo ya mguu.

Beki huyo wa kulia mwenye miaka 29 anayechezea klabu ya Sheffield Wednesday hakuweza kufanya mazoezi na wenzake kutokana na tatizo hilo la mguu.

Pia nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure ambaye hakufanya mazoezi lakini kocha wake Herve Renard anasema baada ya hatua za tahadhari kuchukuliwa kiungo huyo yuko vizuri.

"Ameichezea Manchester City mechi nyingi haswa kati ya Krismasi na mwaka mpya, ila jambo muhimu ni jumanne,"alieleza Renard

Ivory Coast imepoteza nafasi zao mara kadhaa kama timu ilio juu Afrika wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya Algeria na Tunisia.

Haki miliki ya picha Associated Press
Image caption kikosi cha timu ya Ivory Coast

Lakini bado wanajivunia kuwa na kikosi bora chenye nguvu barani Afrika.

Kuwepo kwa ndugu Yaya Toure, kaka yake Kolo, Serge Aurier, Gervinho, Seydou Doumbia na Wilfried Bony kunamfanya kocha Renard kuamini kuwa nyota hawa wa Tembo wa Afrika wanaweza kuukaribia ubingwa.

Mwaka 2012, Renard aliongoza Zambia kutwaa ubingwa,Sasa anataka kukiongoza kikosi chake kutwaa ubigwa.