I Coast vs Guinea:Ukweli wa mambo

Haki miliki ya picha
Image caption Yaya Toure

Hakuna mchezaji ambaye ametoa usaidizi wa mabao katika michuano ya mataifa ya Afrika tangu mwaka 2010 kama Yaya Toure ambaye yuko sawa na John Obi Mikel wa Nigeria.

Toure atacheza katika mechi dhidi ya Guinea akiwa amefunga mabao sita kati ya mechi 8 alizoichezea kilabu yake ya mancity.

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wlfried Bonny alikuwa mfungaji wa mabao mengi katika ligi ya Uingereza mwaka 2014 akiwa na mabao 20 huku yaya Toure akichukua nafasi ya tatu na mabao 17.

Ndovu hao wameshinda mechi tisa na kutoshindwa katika mecho za kimakundi za mataifa ya Afrika licha ya kushindwa kulichukua taji la afrika tangu mwaka 1992.

Kwa upande wake Guinea inaingia katika mechi dhidi ya Ivory Coast ikiwa imecheza mechi nani na kupoteza zengine.