Watson, Ward, Edmund watupwa Melbourne

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mcheza tenesi Heather Watson

Wachezaji tenesi Heather Watson, James Ward na Kyle Edmund wamepoteza michezo na kutupwa nje katika michuano ya tenesi inayofanyika Melbourne Australia.

Ward, ambae anashika nafasi ya pili kwa ubora nchini kwake alipoteza mbele ya Fernando Verdasco kwa jumla ya seti 2-6 6-0 7-6 (8-6) 6-3.

Huku muingereza mwingine Heather Watson akikubali kichapo cha 6-4 6-0 toka kwa Tsvetana Pironkova raia Bulgaria.

Kyle Edmund nae alishindwa kwenda na kasi ya Steve Johnson, kwa kukubali kuchapwa kwa seti 6-4 6-4 6-3 katika mchezo ulitawaliwa na Steve kwa muda mwingi.

Andy Murray ndiye muwakilishi pekee wa Uingereza aliyebakia katika upande wa mchezaji mmoja mmoja baada ya kumshinda Yuki Bhambri wa India.