Tiger Woods apoteza jino uwanjani

Image caption Tiger Woods baada ya ajali ya kamera.

Tiger wood amepoteza jino lake la mbele juu baada ya kugongwa na kamera wakati akimtazama mpenzi wake Lindsey Vonn akinyakua kikombe cha ushindi

Nguli huyo wa zamani wa mchezo wa gofu, aliamua kwenda katika michuano ya kuteleza kwenye barafu ili kumshangaza Vonn mpenziwe ambaye alikuwa hamtarajii kumwona akichuana Cortina d’Ampezzo huko Italia.

Baada ya kuisha kwa michuano hiyo ya kuteleza barafuni, watu wakiwemo wandishi wa habari wakajisogeza karibu na mimbari ya kutolea tuzo ili kutaka kupata picha nzuri ya Woods.

Hata hivyo kulikuwa na msukumano mwandishi mmoja akisukumwa na mwenziwe kiasi cha kuteleza kutoka jukwaani na kamera kumtoka na kumgonga Tiger Woods mdomoni,na wakala ya nguli huyo wa zamani wa mchezo wa golfu alieleza hali hiyo kuwa aligongwa kwa bahati mbaya