De Gea, Reid, Schurrle,Fletcher wawindwa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kipa wa Manchester United David de Gea

Manchester United imesema kipa wao David De Gea, anathamani ya Dau la Pauni milioni 50, Kipa huyo amekuwa akiwaniwa na miamba wa Soka wa Hispania Real Madrid.

Mlinzi wa kimataifa wa Ujerumani Matts Hummels amezikatisha tamaa timu za Man Utd, Liverpool na Chelsea zinazomuwania kumsajili kwa kusema anataka kusalia na klabu yake ya sasa ya Borussia Dortmund.

Beki wa West Ham Winston Reid,amesema hatosaini mkataba mpya na timu hiyo na anataka kujiunga na washika bunduki wa London wa Arsenal.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mshambuliaji wa Chelsea,Andre Schurrle

Klabu ya Wolfsburg iko tayari kutoa pauni milioni 23 ili kupata saini ya mshambuliaji Andre Schurrle, mwenye miaka 24 toka Chelsea japo timu yake inataka pauni milioni 30 ili kumuachia mchezaji huyo.

Kiungo wa Arsenal Francis Coquelin, anajiandaa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo baada ya kufanya vizuri tangu atoke Charlton Athletic alikokuwa anacheza kwa mkopo.

Kiungo wa Manchester United Darren Fletcher,anaweza kujiunga na timu ya Valencia ya Hispania japo kuwa timu ya West Ham imeonyesha nia ya kumsajili kiungo huyo.

Timu ya West Brom wako tayari kumpa mshambuliaji Saido Berahino mshahara mara mbili ya anaotapa sasa lli aweze kusalia na klabu hiyo.

Mshambuliaji aliyekosa nafasi katika kikosi cha Tottenham Roberto Soldado, anatakiwa na klabu ya Bayer Leverkusen.

Timu ya Stuttgart imekataa ofa ya pauni milioni 5.5 iliyotolewa na Swansea ili kuweza kumsajili kiungo Alexandru Maxim.

Manchester United inajiandaa kutoa dau la pauni milioni 15 ili kumrejesha beki Gerard Pique, aliyewahi kuichezea timu hiyo lakini hakufanya vizuri.