Arsenal yamsajili Krystian Bielik

Image caption Krystian Bielik aliyesajiliwa na Arsenal

Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 kutoka kilabu ya Legia warsaw kwa kitita kisichojulikana.

Bielik aliichezea timu kubwa ya kilabu hiyo ya Poland mnamo mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 16.

Pia alishiriki katika mechi tano ya kilabu hiyo na mara moja katika ligi ya yuropa.Mchezaji huyo anayesifiwa na wengi anaweza kucheza katika safu ya kati na ile ya Ulinzi.