Burkina Fasso yaapa kuwashinda wenyeji

Image caption Afcon

Nahodha wa timu ya taifa ya Burkina Fasso Charles Kabore amesisitiza kuwa wataimarisha mchezo wao baada ya kushindwa na Gabon katika mechi yao ya kwanza.

''Mashindano haya hayajakamilika kwetu sisi.''Iwapo tutashinda dhidi ya wenyeji wa maandalizi haya basi kila kitu kitakuwa shwari''.

Mkufunzi wa timu ya Equitorial Guinea Esteban Becker anajua kwamba timu yake ni sharti ishinde mchuano huo dhidi ya Burkina Fasso ilio na washambuliaji mahiri.

Hatahivyo Equitorial Guinea ni sharti iimarishe safu yake ya Ulinzi,baada ya kushindwa kuweka rekodi ya kutofungwa katika mechi zake nne katika michuano hiyo.