E Guinea yatoka sare na Burkina Fasso

Haki miliki ya picha
Image caption Equitorial Guinea

Burkina Fasso wamepiga chuma cha goli mara mbili na hivyobasi kuzuiwa na Equitorial Guinea katika sare ya kwanza ya 0-0 katika michuano ya mataifa ya Afrika.

Alain Traore aliupinda mkwaju wake dhidi ya chuma cha goli kunako dakika ya 19 na 20 kabla ya mkwaju wake kupigwa nje na mlinda lango wa Equitorial Guinea Didier Ovono.

Wachezaji wa Burkinabe pia karibia wafunge baada ya kipindi cha kwanza wakati Jonathan Pitroipa aliposhindwa kufunga krosi .

Mchezaji wa Equitorial Guinea Doualla alikosa bao la wazi alipopiga juu akiwa katika eneo la hatari.