Gervinho aomba msamaha kwa kadi nyekundu

Image caption Gervinho

Mchezaji wa Ivory Coast Gervinho ameomba msamaha baada ya kupewa kadi nyekundu kwa kumpiga mlinzi wa timu ya Guinea Naby Keita katika mechi ya timu hizo mbili ilioisha 1-1.

''Nataka kuomba msamaha kwa taifa la Ivory Coast,wachezaji wenzangu na waandalizi wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa kitendo hiki cha hasira'',aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

''Haikuwa mimi na vitendo kama hivyo havina nafasi katika viwanja vya soka'',,aliongezea.

Kulingana na sheria za FIFA, mchezaji hukosa mechi moja anapopewa kadi nyekundu ,lakini shirikisho la Soka barani Afrika huenda likaongeza adhabu hiyo.

Kawaida mtu hupewa marufuku ya mechi mbili katika michuano ya Afrika,lakini adhabu hiyo inaweza kuongezwa na kufikia mechi nne iwapo kamati ya nidhamu itahisi mchezaji huyo anahitaji kupewa adhabu kali.