Ronaldo:Sitojiunga na Man U ama Chelsea

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mchezaji wa Real Madrid Ronaldo asema hatojiunga na Chelsea wala Man United

Mchezaji bora duniani kutoka kilabu ya Real Madrid Christiano Ronaldo amewavunja moyo mashabiki wa kilabu ya Manchester United na Chelsea baada ya kusema kuwa anapania kwenda Brazil kusakata kabumbu baada ya kutoka Real Madrid kulingana na gazeti la Metro.

Mchezaji huyo ambaye anatabiriwa na wengi kurudi katika kilabu ya Manchester United baada ya kumaliza mkataba wake na Real Madrid amesema huenda akaichezea kilabu ya Corinthians ama hata Flamengo nchini Brazil atakapoondoka Real Madrid.

''Corinthians na Flamengo ni vilabu maarufu ambavyo huenda nikachezea moja wapo.nchini Brazil nina marafiki wengi kwa hivyo uhusiano wangu na taifa hilo ni mzuri sana.''alisema Ronaldo.