Tanzania kumenyana na Rwanda leo

Image caption Taifa stars maboresho

Timu ya Tanzania, Taifa Stars leo inakabiliana na majirani zao Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa katika mji wa Mwanza magharibi mwa Tanzania.

Akizungumza na BBC, mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania, TFF, Boniface Wambura amesema maandalizi ya mchezo kati ya timu mbili hizo yanaendelea vizuri ikiwa pia ni fursa kwa timu hizo kujiandaa na mashindano yajayo ya Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, yanayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi zao maarufu kama CHAN.

Rwanda ndiye mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.

Timu ya Rwanda pia imo katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza michezo ya Olympiki ya Rio De Janeiro nchini Brazil mwaka 2016.