Real Madrid,Man U zaongoza kwa utajiri

Image caption Kikosi cha Real Madrid

Mabigwa wa ulaya klabu Real Madrid ya Hispania imeendelea kuwa kuwa timu tajiri Zaidi duniani

Takwimu zilizotolewa na Deloitte, ambao ni Wataalam wakubwa wa Mahesabu Duniani zinaifanya Real Madrid kuendelea kukaa kileleni mwa vilabu tajiri Zaidi.

Manchester United wanashika nafasi ya pili katika listi hii wakipanda kutoka nafasi ya nne,huku mapato ya mwaka 2013/14 yakitumika kama kigezo.

Timu kumi za mwanzo zote zinatoka katika ligi tano kubwa barani Ulaya almarufu kama (Big Five) ambazo ni ligi kuu ya England, Ligi ya Hispania La Liga, Bundesliga ya Ujerumani, Serie A ya Itali, na Ligi 1 ya Ufaransa.

Ligi England inaoneka ina utajiri zaidi kwa kufanikiwa kuwa na jumla ya timu tano katika kumi bora.

klabu ya Galatasaray ya Uturuki ndio timu pekee iliyongia katika ishirini bora ikiwa haimo kwenye timu zinazotoka kwenye ligi tano bora.

Msimamo kamili ni kama ifuatavyo kwenye mabano ni kipato cha mwaka 2012-2013

1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)

2. Man United: 518m (423.8m)

3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)

4. Barcelona: 484.6m (482.6m)

5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)

6. Manchester City: 414.4m (316.2m)

7. Chelsea: 387.9m (303.4m)

8. Arsenal: 359.3m (284.3)

9. Liverpool: 305.9m (240.6m)

10. Juventus: 279.4m (272.4m)