Arsenal yafanya mazungumzo na Paulista

Haki miliki ya picha z
Image caption Paulista kushoto

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kilabu yake imeanza mazungumzo na mlinzi wa wa Villareal Gabriel Paulista.

''Mazungumzo yanaendelea vyema''alisema.

''Hatahivyo sijuia kama tutaafikia makubaliano,lakini tuna fursa ya mafanikio''.

The Gunners italazimika kumtafutia cheti za kufanyia kazi mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24.

Arsenal imemsajili Krystian Bielik kutoka kilabu ya Legia warsaw kwa kitita cha pauni 2.4 wiki hii.

Wenger alisema kuwa Bielik ambaye anaweza kucheza katika safu ya kati atatumiwa kama kiungo wa kati wa ulinzi.