Ligi kuu Tanzania kuendelea Jumamosi

Image caption Timu kadhaa kujitupa uwanjani Jumamosi ligi kuu Tanzania

Ligi kuu ya Tanzania itaendelea Jumamosi hii huku mechi kadhaa zikichezwa ikiwemo ile kati ya bingwa mtetezi na wawakilishi wa nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Azam FC na Simba Sports Club ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic.

Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 20 na baada ya mechi yao na Simba itaenda Jamhuri ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kucheza mechi za majaribio kwa ajili ya mechi yao na vigogo wa Sudan, El-Merreikh katika mechi ya kwanza klabu bingwa Afrika itakayochezwa Dar es Salaam kati kati ya mwezi ujao.

Mabingwa wa zamani wa Tanzania na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga, ikiwa ya nne katika msimamo na alama (points) 15, watacheza na Polisi Morogoro wakati Mtibwa Sugar, ikiwa ya pili na alama 17, watacheza na Ruvu Shooting.

Mechi nyingine ni kama ifuatavyo

Stand United vs Coastal Union-Uwanja wa Kambarage,Shinyanga

Kagera Sugar vs Ndanda-Uwanja wa Kaitaba, Kagera

Mbeya City vs Tanzania Prisons-Uwanja wa Sokoine, Mbeya