Man U sare na timu ya daraja la pili

Haki miliki ya picha empics
Image caption Nahodha wayne Rooney Louis Van Gaal

Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa kila kitu kilikwenda kinyume na matarajio ya timu hiyo wakati wa sare ya 0-0 dhidi ya timu ya Cambridge United katika kombe la FA raundi ya nne.

Radamel Falcao na Angel Di Maria wote walikosa mabao katika uga wa Abbey.

Lakini kikosi cha Van Gaal kilishindwa kuibwaga miamba hiyo ya ligi ya daraja la pili na kulazimika kukutana nao tena nyumbani Old Trafford.

''Kila kitu kilikwenda kinyume na matarajio yetu,si uwanja refa ...yani kila kitu'',alisema Van Gaal.